Road pt.2: HOME - SWAHILI LYRICS

*Translation by Moige (IG@moige.pd)

Tupoteapo njiani 

Ni rahisi kusahau nyakati za furaha 


Na saa zingine, tunadhani 

Kusonga mbele ni kusahau 

na ni kupoteza njia ya kurudi nyumbani 


bali tunakubali


popote ulipo 

au ndoto zako zinapobadilika 

na mipango yako yasipofanikiwa 


na ikiwa njia yako 

imejawa matatizo

yaliyokusababisha kuaibika


angalia kwa makini

na utaelewa

barabara za kuenda

ni za kurudi pia 


nyakati huzidi kubadilika 

na hisia zetu hugeuka kuwa tofauti 

ingawaje, upendo na tumaini hudumu


maishani kuna huzuni na furaha pia 

kwa haya yote, sitakuacha

kumbuka, kuimarika huitaji kulia 


bali tunakubali


popote ulipo 

ndoto zako zinapobadilika 

na mipango yako yasipofanikiwa 


na ikiwa njia yako 

imejawa matatizo

yaliyokusababishia aibu


tazama

na utaelewa

barabara za kuenda

ni za kurudi pia 


kurudi nyumbani 


usife moyo 

utarudi nyumbani 


popote ulipo 

ndoto zako zinapobadilika 

na mipango yako yasipofanikiwa 


na ikiwa njia yako 

imejawa matatizo

yaliyokusababishia aibu


tazama

na utaelewa

barabara si tu za kuenda

hatutatenganishwa kamwe 

unahitaji tu kurudi nyumbani 


rudi nyumbani 


rudi nyumbani 

** You don't see the translation in your language and you want to contribute with translating it? You can now do it, you'll just need to fill out this form 
EmailSpotifyYouTubeTwitterInstagramTikTok